Burundi Transparence
main image
shadow shadow

 

Hadji Hussein RADJABU mkutanoni

Injini ya CNDD-FDD Hussein RADJABU kuzulumiwa nafasi yake, kumtenga tuu na chama kufifia. Ufahamu kwamba chama kilivyo kuwa kikizama anakiokowa, mnamo mwaka wa 1994-1995, kulianzishwa mchakato wakutetea wanyonge ambao ni raia wa inchi ya Burundi.

Bwana huo Hussein RADJABU tunaweza kumwita kuwa ni SIMBA WA VITA vya msituni, alikuwa akishughulika na kazi ya ukamishna mkuu anaeshughulikia mambo ya propaganda ; akiwa yeye ndo ana angalia mambo yote na kuyapanga, sababu kulikuwepo viongozi wa chama wakiongozwa na Bwana Leonard NYANGOMA kipindi hicho, wote wakihofia usalama wao inchini walikuwa wakieshi uhamishoni.
Simba huo wa vita yeye peke yake aliweza kukusanya vijana kwenye uwanja wa mapambano nchini na kuwa anapeleka ripoti kwa viongozi hao wangazi za juu uhamishoni.

Moto wa vita wa mwaka 1994-1995, Simba wa vita Hussein RADJABU alifaanikisha kupanga safu za wapiganaji na safu za wana siasa, majeshi makuu akiwemo col. Jean-Bosco NDAYIKENGURUKIYE, col. MBAWA, Major NGURUBE, comdt. Laurent, na wengine wote hao walimkubali simba huo wa vita kwa mipangilio yake.

Ila huku wanasiasa waliokuwa uhamishoni akiwemo mwenye kiti NYANGOMA Leonard, kwa uchu wa madaraka waliona kama vita vinawakawiza ndipo walianza kudumbukiya kwenye mtego wa adui, mwaka wa 1998,mambo ya kaanza kuwa magumu kwenye uwanja wa mapambano huko Zaire ya zamani vita vikipamba moto.

Simba wa vita Hussein RADJABU akatumiya ushuja wake na kuweza kumfikia kiongozi wa kipindi hicho Bwana Leonard NYANGOMA ila kiongozi huyo akakaidi ushauri aliopewa, na kuzama kwenye dimbwi. Hussein RADJABU akawahi kwenye uwanja wa mapambano na kuwapa hali halisi majeshi na wengine wana siasa wakachukuwa uamuzi wakufanya mabadiliko.

Ndipo Col Jean-Bosco NDAYIKENGURUKIYE alipo chukua uskani wa kuwa Mwenyekiti, huku Hussein RADJABU akafanywa Katibu Mkuu wa chama. Adui akaona vijana wanarudi kwenye mstari mzuri uwanjani. Akaunda mbinu kali zaidi akapitia kwa simba huo Hussein RADJABU ikashindikana. Huku mazungumzo yakiwa yalianzishwa nchini Gabon.

Viongozi tena wa ngazi za juu kupiitiya Mwenyekiti wao Jean-Bosco NDAYIKENGURUKIYE kwa uchu wa madaraka na kuwahi vyeo nchini, ndipo
wakapoteza msimamo, nakuwahi kujitowa Katibu Mkuu ambae ni simba wa vita kwa kumteuwa kuwa Mshauri wa mwenyekiti yaani Jean-Bosco NDAYIKENGURUKIYE hayo wakiyafanya ili simba asiweze kujuwa kinacho endelea. Ndipo Simba akaanza kuona wanapangua watu wote wenye msimamo akawahi kuonana na wanyonge ambao ni raia, na kuwaeleza hali halisi kuwa viongozi wamekwisha tupa mstari, wakiwemo Leonidas HATUNGIMANA (Chos) kamanda wa oparesheni, Wagara Melchior na wengine, ndipo raia wakamuomba haraka sana aweze kuchukuwa uskani yeye mwenyewe.

Simba wa vita Hussein RADJABU kama kawaida yake yakutopenda vyeo
na madaraka, alipendelea makamo wake wa ukatibu mkuu bwana Peter NKURUNZIZA aweze kuwa mwenyekiti ; wafwasi wa chama wakapinga hatuwa hio. Ndipo simba akawaelewesha kuwa watasaidiyana wote kwenye mikikimikiki ndipo NKURUNZIZA kukubalika na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti, Simba wa vita akabaki kuwa katibu mkuu wa chama Cndd-Fdd.

Hapo Hussein RADJABU akasimamia mazungumzo ya kusitisha mapigano hadi kufikia kwenye mkataba huo wa amani. Wakaingia nchini, vyeo walivyo pewa Hussein RADJABU akakataa cheo hata kimoja kwa kuhofia chama kisiwe kama kilivyokuwa kipindi cha nyuma. Lengo la Simba huo wa vita, ilikuwa ni kukamilisha kiu cha wanyonge ya muda mrefu kutaka waeshi kwa amani na kujiamini.  

Ndipo uchaguzi ulivyofika chama kikawa kimemteuwa mwenyekiti wake kugombea urais na hapo kumchaguwa simba wa vita kuongoza chama. Chama kikashinda uchaguzi kwa asilimiya nyingi tu, Nkurunziza akawa Rais. Adui akaona sasa atapenya vipi ; kupitia chama yuko Simba huo.  

Ndipo walitumiya mbinu zao zote kwa kupitia ile ile njia ambayo huwa mara kwa mara wanapitia ikiwa sio simba yuko kwenye uskani ndipo Rais Peter mtegoni bila kujuwa ametoka wapi? Na anakwenda wapi? Huku majenerali kama Adolphe Nshimirimana, Alain Guillaume Bunyoni, Evariste Nshimiye, katibu mkuu wa chama nae ni Manace Nzobonimpa, Speaker wa senet na baadhi ya ma senator na wabunge wote hao wakajikuta wameingiya mtegoni mwa adui, kwakuwa wote hao walipandikiza tamaa mbele, pili wakapenda vyeo, tatu kutokuwa na busara.
 

Adui akatumia kigezo cha kuwadanganya kama watoto, hata mwendawazimu yaani msazi hawezi kudanganywa hivyo, lengo lake amkimbize Hussein RADJABU sababu ni muona mbali. Ili lengo lake alifikie bila matatizo ndipo uongo ukawa mwingi kutumia hata vyombo vya habari eti Rais hauhukumu inchi, nchi inahukumiwa na mwenyekiti wa chama tawala, ukizuba atakutowa kwenye hiyo nafasi yako, akisahau kuwa kachaguliwa.  

Ndipo kundi lote hilo lenye tama likatumia kuvunja katiba na sheria kwa kumtowa simba huo Mhesh. Hussein RADJABU kuongoza chama tawala. Ikaonekana anakubalika na wanyonge ambao ni raia, wakachukuwa jukumu laku mtowa duniani, ila Mwenyezi Mungu akasema huna hatia baki kwenye ardhi yangu, wakaona hawawezi kumtowa kwenye ardhi ya Mungu wakapendelea kumtowa kwenye ardhi ya kuonana na raia ; ndipo kuchukuwa uamuzi wakumtia mbaroni Mpimba.

Rais mtego ukawa umemnasa haswa akaanza timuatimua kila anae uhusiano na mwenyekiti huo Hussein RADJABU, maskini ya Mungu akajivutia karibu yake wale ambao walikuwa waliasi enzi za vuguvugu la kufikia kwenye wako hivi.

Nao ni kama hawa wafwatao : Hatungimana Leonidas(chos) hivi ni msemaji wake, ikumbukwe kuwa huo Chos alitowa ahadi kuwa atatia adabu wale wote waliompinga kiongozi wao kipindi hicho Bwana Jean-Bosco Ndayikengurukiye, mwengine ni Wagara Melchior, nae alikuwa anaenda kwenye uwanja wa mapambano kuhamasisha iliwamfwate J.B. Ndayikengurukiye, mungine ni Moise (Padiri) bila kusahau mzee Ndarubagiye Leonce mfwasi wa Leonard Nyangoma wote hao ivi ndiyo wanashika hatam katika ikulu ya Peter, lengo kujilipiza na kuwahi kujipapulia sababu hawana hamu yakutetea wanyonge.

Si inaonekana kuwa Rais katekwa ? Na Adui anajipatia njia kiurahisi. Chama chazidi kudidimia, inchi yawa hatarini kukosa muelekeyo.  

HIVI WANAKUMBUKA WALIOJITOWA MUHANGA ILI WAFIKIE HAPA WALIPO SASA??

 
Mshirika katika mapambano

 

 

horizontal bar

 

Burundi Transparence © 2007