Burundi Transparence
main image
shadow shadow

 

SURA YA CHAMA CNDD-FDD LEO   Le 28 août ‘07

Tarehe 26/August/2007 miaka miwili ya ushindi wa chama tawala  cndd-fdd

Tarehe27/August/2007 Miezi Minne simba wavita vya msituni akingurumia jela kuu la Mpimba El Hadj Hussein Radjabu.

TArehe07/Febr/2007.Siku yatukio lililosambaratisha Chama ca cndd-fdd.Tarehe hizo hazitosahaulika kwa kuwa kinara wa chama hico Hon El Hadj Hussein Radjabu alipo  pokonywa  madaraka yakuongoza Chama ca cndd-fdd .Kinyume cha sheria za chama  na za nchii , zowezi hilo likisimamiwa na waziri  wa mambo ya ndani jenerali Evariste Ndayishimiye kwa kupana ruhsa ya kongamano kharam kufanyika Ngozi tarehe 7-febr-2007.

Badaa ya hapo ndipo shutma na Hila  za hapa napale zikaanza kubuniwa.

Vitimbi alivyo tendewa kinara huo nikama vifwatavyo :

1-Alipokuwa akenda nchiini kati hufwatiliwa na Jeshi la Polisi na Idara za Upelelezi.

2-Alipokuwa akifika mahali huziwiliwa kuzungumza na wanachama.

3-Inapofikia wafwasi wake kumlaki hupigwa nahatabadhi hutiwa korokoroni.

Hayo yote yalikuwa yakifanyika Rais akisalia kimya,huku nae akiwa ni mwanachama.

Sintofahamu hiyo iliendelea hadi tareh 27/04/2007. Ndipo Kinara huo na Simba wa Vita vya Msituni Hon EL Hadj Hussein Radjabu  Jioni aliingizwa Jela kuu la Mpimba,Bujumbura.

Leo tareh kama hiyo 27/08/2007 Ndipo kinara huo ametimiza Miezi minnee(4) bila ya kufunguliwa Mashtaka yoyote yale.Pamoja nakuwa hapo kabla alikuwa akishtumiwa makosa kadhawakadha. Ila kwasasa shutma zote zimegeuka upepo na kupeperuka. Nakuacha kitendawili katka viongozi wa nchi hii,na wale wa Idara za Upelelezi,na Hakimu Mkuu wakiwa njiapanda bila kujuwa lakufanya,iliwaweze kupata lakudanganya wananchi na jamii la kimataifa,ambao wanaskilizia kwa makini kinacho endelea.

Visa na mikasa havikuishia hapo. Akiwa huko ndani ya Jela  kuu la Mpimba Kinara huo kwanza.1- Aliziwiliwa chakula na Maji.

Pili :  2-Alifungwa katka chumba cha pekee kisichokuwa na dirisha.

Tatu: 3-Alinyimwa haki zakutokutoka nje kuonana na wafungwa wengine, kwamadai ya kwamba  atahatarisha usalama katka jela hilo.

Nnee : 4-Alisachiwa kwa madai ya kwamba anamiliki vyombo vya mawasiliano ndani ya jela

Tano : 5-Majaribio ya kummalizia maisha yalio pelekea kumvunjia mlango na kuingiza askari Polisi wakiwa na silaha ndani ya chumba chake usiku.

Hatujataja kutolewa Jela jioni na kupelekwa kwake,ashuhudie ginsi familia yake inavyo zalilishwa na maPolisi,kwa kuporwa mali zake. Na hapo ndipo wakili wake NIYOYANKANA Prosper alipopewa mkong’oto wanguvu nakutupwa korokoroni mda.

Mkasa wote huo ulikuwa chini ya uratibu wa Afisa wa Jeshi la Polisi Colonel GAHUNGU Bertin Kamishna wakitengo cha Ughalifu.Hayoyote ikiwa ni kinyume cha Sheria.

Istoshi Huwa kinara huo alikuwa akiletwa Mahakamani safari zisizokuwa na mpango,kwa kuzuga Raia na Jamii la kimataifa,bila ya kumuhoji lamaana lolote.

Hapo tena wafwasi wa kinara huo wanapo fika Mahakamani,hupigwa na kudhalilishwa na Jeshi la Polisi wanaongozwa na Kamanda NIKIZA David.

Hayo yote nayo pia huwa yalikuwa yakifanyika Rais akisalia kimya.

Waswahili wasema hakuna marefu yanayo kosa ncha.

Dhamira za ukimya wa RAIS zime dhihirishwa na Skuku ya Ushindi wa Chama cha CNDD FDD kuzigeuza Skukuu yake binafsi,na baadhi ya wafwasi wake na wale wanaotetea maslahi yao ya kazi,wasio juwa niginsigani wanachama walivyopata shida kwa kukifikisha chama madarakani.Ayoyote ni ishara tosha ya uchu wa madaraka aliyo nayo Baba wa Taifa. Akisahau kama chama hicho ndo kilichofkisha madarakani.

Hapo ndipo mtu anaweza kujiuliza maswali,je ushindi wa chama umegeuka wa mtu binafsi ?!

Ao dhamira ya Rais nikuhakikisha chama amekizika kabisaa.Iliaweze kufunguwa Parokia kijijini kwao,akijuwa kwamba hakuna chama kitakacho mbugudhi.

Ikumbukwe yakwamba siku kuu hiyo ya ushindi wa chama cha CNDD-FDD, wana chama walivyo kuwa wakishirikiyana  kwapamoja na kinara wao Hon El Hadj Hussein Radjabu kwa shangwe  na kupongezana na kushauriana na kusameheyana, na kukumbushana niginsi  gani waimarishe chama chao kwa pamoja.

Leo tumetazama matukio muhimu katka kipindi hiki cha miezi mi nne ya kifungo cha Simba wa vita vya msituni na kuazimisha miaka miwili ya ushindi wa chama tawala. Toleo lijalo litawamulikia miezi mi sita yakutokuwepo madarakani kinara na shuja,Mwanga  na muongozo Simba wa vita vya msituni Muheshimiwa Hon El Hadj Hussein Radjabu na maisha yake ndani ya vuguvugu la CNDD na baadae kuwa CNDD-FDD kabla ya mazungumzo yalio pelekea ustishwaji vita na kupelekeya kuwa chama

 

Burundi Transparence

 

horizontal bar

 

Burundi Transparence © 2007