Burundi Transparence
main image
shadowshadow

 Habari

 

Je nilini Raisi Peter Nkurunziza aliamua kutumia uhariri wa Burundi News kama mbinu za kumng’atua Radjabu ?
Tarehe 22 Mei 08

Mwandishi: Gratien Rukindikiza

Ni vigumu kuamini lakini ni kweli yametokea. Raisi Peter Nkurunziza aliamua kutumia tovuti Burundi News ili aweze kusambaza habari za Kashfa dhidi ya Radjabu, vile vile nakujiandalia ung’atuzi wake. Toka mwisho wa mwezi disemba 2006, ndipo tovuti Burundi News ilianza kuandika habari nyingi navile vile kuwa chazo cha habari zinazo andikwa na vingine vyombo vya habari kuhusu mifarakano ilio ripuka ndani ya chama tawala.

Wengi walifikiria kwamba raisi hajuwi lolote kuhusu yalio kuwa akitendeka. Wengine eti anatumiwa na Radjabu. La hasha ! haikuwa hivyo. Kwa muda mrefu raisi alikuwa na njama za kumng’atua Radjabu, lakini ilikuwa siri aliyo ficha uongozi wa chama cndd-fdd. Na aliacha baadhi yavikundi kuanda mpango huo ili alaghai kama yeye hausiki na mpango mzima wa kumng’atua Radjabu.

Uamuzi wa kushirikisha Burundi News

Mkutano uliyofanyika chini ya uongozi wa raisi ili wajiandae kufahamisha wafuasi wa cndd-fdd, hatua waliofikia ya kumng’atua madarakani Radjabu. Mkutano huo ulishirikisha raisi Peter, Gen Adolphe Nshimirimana na Muhammed Rukara. Katika mkutano huo ndipo walipo amua kuchukua uamuzi wa kutuma habari katika uhariri wa tovuti (Website) Burundi News, ili waweze kuzitangaza. Vile vile walipanga mbinu za kuficha chanzo cha habari hizo. Watatu hao ( Peter, Adolphe na Rukara) waliteuwa mtu wakutufikishia habari hizo. Sisi waandishi wa tovuti Burundi News tuliona habari hizi si za kawaida ili tuweze kutambua undani na ukweli. Tangu tupate taarifa za mwanzo tulifanya upelelezi nakutambua kwamba kuna mpango wa kumtoa madarakani Radjabu.

Chanzo chetu cha habari, alitupasa kumuamini kwani habari habari aliekuwa akileta zilikuwa sahihi.

Wasiwasi kati ya wanachama

Toka tuandike habari zamwanzo zilizua wasiwasi mkubwa kati ya wafuasi wa chama hicho kwa kua hawakuweza kuelewa ni nini kinachoendelea. Baadhi walijitahidi kutukosoa lakini walizidiwa kwa hiyo waliamua kuachana navyo. Wengine nao waliendelea kupeleleza ili wajue kama habari hizo ni ukweli au la ! Kwa mfano, wawakilishi wawili wa chamahicho (cndd-fdd) barani ulaya walioulizia makao makuu Bujumbura kuhusu ukweli wa habari hizi, hawakupewa jibu sahihi , bali waliambiwa wasome tovuti Burundi News.

Tangu habari ya mwanzo mpaka ya mwisho, zote zilitumwa na watatu hao (Peter, Adolphe na Rukara).

Wasiwasi kati ya waandishi wa tovuti Burundi News

Mwanzoni tulifikiri kwamba ni mtu anaefahamu siri kati ya Radjabu na Nkurunziza nakuhisi ana mwenendo wa ndumilakuwili. Ilifika wakati nasi tukakunwa na machale, tukaamua kupeleleza zaidi. Siku moja tukapata simu kutoka Bujumbura kwa rafiki yetu akisema : « Habari hizo ni sahihi lakini wanaozifahamu Bujumbura niwachache ». Taarifa hiyi ilitushangaza sana. Aliendelea akisema kwamba anaesoma habari zenu na akawa anawafahamu wanasiyasa wetu moja kwa moja anaweza kutambua kwamba habari hizo zinatoka kwa raisi Nkurunziza kwa maana sioni mtu mwengine anayeweza kupata habari hizo katika wakati mgumu kama huu. Nahapo ndipo tulipojua ukweli ni upi japokua tulijua siri tuliamua kuilinda ; baada ya mwaka Hussein akiwa yupo kiziwizini twamua kuyaweka mambo bayana.

Habari zingine

Radjabu hakufahamu walikuwa wakimchezea. Siri iliovuja kutoka ikulu, ilieleza kwamba kuna maandalizi ya kumtwisha mzigo Radjabu lakini hakuna aliyempatia taarifa hizi. Zile faili zakutisha kama kupindua serikali, uuzaji haramu wa Falcon 50, mauaji ya kinyama yaliotokea Muyinga na Kinama ; hayo yote wakapanga kuyatwisha Radjabu.

Pia wakazagaza nchini na inje ya nchi yakwamba mambo yanaenda kombo nchini kwa sababu ya Radjabu. Kaseti yakusikiliza ilioundwa ashutumiwe na makosa yakupinduwa serikali na kuhatarisha usalama wa nchi, ilitengenezewa ikulu. Wakati huo habari zilizotangazwa na RPA hazikuwa na msingi. Anaeongoza idara ya upelelezi (Adolphe Nshimirimana) ndiye aliekabidhi kaseti hiyo RPA kwa idhini ya raisi. Kung’atulia madarakani na kuwekwa kiziwiziwi kwa Radjabu vilirahisishwa na uchochezi wa Redio zilizosambaza kashfa za uongo juu yake. Wanaofikiria kwamba Peter Nkurunziza hana mipango, wanaowaza kwamba anatumikishwa wanajidanganya sana. Leo hii kuna majenerari wanaofikiria kwamba kabla Raisi hajashika uwamuzi anawaomba ushauri nawao wanajidanganya sana ; wasubiri kesho Raisi atachochea redio majenerari hao wapakaziwe mpaka waonekane hawafai.

Ujumbe kwa Raisi

Kwa kazi tuliyowafanyia, si vema kwako kuomba nirudishwe nchini kuja kuhukumiwa, mtatuhitaji kuangusha jenerali yeyote anayowasumbua. Tunaamini kwamba kazi tuliowafanyiya ni ndogo mno ikilinganishwa na wema aliyokufanyia Radjabu kuwakalisha kwenye kiti cha ufalme nawe ukamlipa gereza. Hatuombi shukrani kutoka kwenu, ila tunaomba umtendee haki Radjabu, umshike kama binadamu. Pia tunaomba uwape usalama wanainchi waburundi.

 

Burundi Transparence

 

horizontal bar

 

Burundi Transparence © 2008