Nani anayetaka kumtambuwa Muhamed Rukara (sehemu
ya pili)
Le 27 avril ‘07
katika ukurasa wa kwanza tuliwahakikishiya ufedhuli na umaluhuni wa
bwana M.R na kuwaahidi kwamba atapozidi kupewa na fasi naye atazitumiya kwa
maslahi yake lakini mpaka lini?Bwana huyu aliyeteuliwa na Rais wa nchi
katika baraza la wazee wa hikma na busara wa chama cha cndd/fdd ya
ngozi,kajifanya siku hizi kuwa na maelewano ya kutosha na mkurugenzi mkuu
katika idara ya upelelezi.sasa hivi offisa huyu anamsaidiya katika kutumiya
luhga za uongo na vitisho na ndiyo urahisi aliwahi kutumiya kwa
kujiheshimisha kwenye jamii ya kiislam hapa nchini.hivi sasa anaonekana
kuwa mchezaji mzuri wa golf na tennis akigeuza raketi zake kwa wafanyakazi
wa serikali na idara zake akiwahakikishiya wawe na msimamo wa kujiteteya
ikwa rais atajaribu kuwafuta kazini,kama vile kuteuliwa kwa naibu
mkurugenzi wa bandari ya bujumbura Nsabimana Yakubu ambaye mama yake
aliposhahidiliya alikuwa anaeshi katika familiya ya Mzee Rukara
Khalfani.kwa hiyo huyu kijana aliyeteuliwa pamoja na bwana Henry le
page mkurugenzi mkuu wa Sobugea(inashughulikiya mapokezi,usafirishaji na
uwekaji wa mizigo)kwenye aeroport international ya bujumbura na
anaefahamika vema katika jamii ya warundi huko bruxelles na ulaya
pote,mabwana hawa wawili wanalazimishwa na M.R kutowa kila mwisho wa mwezi
kitita sawa na miliyono moja pesa ya burundi akidayi kuwa ni kinga kwao na
kuwaepusha kufutwa kazi, na haitoshi huyu Lepage akimlazimisha
kuwatembeleya raia sehemu fulani fulani akiwakubaliya kuwapatishiya kazi
kwenye idara hiyo ya sobugea sababu wanamuona yupo pamoya na meneja, pia
alimlazimisha huyu bwana Nsabimana yakubu kukodi nyumba yake iliko katika
tarafa ya kinindo barabara ya ntwarante.
siku ya ijumaa tarehe 13/april/07mwana mama katibu mpya mtendaji wa
mairie wa bujumbura aliachana na mumewe vibaya akimshutumu vitendo vya
ufedhuli huenda na zina na bwana M.R huku akidayi kuwa alimsaidiya
kumpatishiya kazi hiyo pindi walipoanza kufutwa viongozi mbali mbali na
rais kwa kuwa wana harakati wenye msimamo kwenye sheriya na haki wakitwa
kwa lugha nyingine Pro-Radjabu.mwana mama huyo ni mwenye saili ya tarafa ya
buyenzi barabara ya 4 n°7 lakini alikuwa anaeshi tarafa ya nyakabiga na
mumewe.
bwana M.R na nduguye Idi kabano mkuu wa tarafa ya buyenzi wamejipa
shughuli ambayo kwa kweli huenda ikawadhuru hivi karibuni wakijiunga na
baadhi ya vijana wenye uroho na njaa kali kuwatafuta hasa waislam
wanaodiriki jamaa miskiti miwili ya barabara ya 5 buyenzi,ili wawataje watu
ambao bado wanamteteya mbunge Hussein Radjabu na kuwakubaliya kuwapa
faranga elfu tano ukiwapata wawili na faranga elfu kumi utapomkamata sehemu
za barabara ya 20av n°48 panaitwa maarufu(Kijiweni).
na haitoshi wamekwisha weka majasusi katika mitaa yote ya kiislam nchi
nzima na habari za kuaminika inawezekana kuwa wamepewa ruhsa kutoka ikulu
kuwawinda waislam wote wanao jaribu kusema ukweli wakiitwa ni waRadjabu
Hussein, jumapili tarehe08/04/07.bwana M.R,aliitisha kikao cha body yake cha
watu kumi akiwemo idi kabano,hamza burikukiye,muhamed nibaruta na muhamed alamin
na wengineo nyumbani kwake kabondo,mkutano huwo umeanza saa tatu asubuhi na
kumalizika saa sita mchana,agenda ya mkutano huwo ilikuwa kijifunza namna ya
kuigeuza ao kuongeza katika katiba ya Comibu na kuanza mikakati ya mngatuwa mkuu
wa Comibu ambaye ni Sheikh Salum Issa na kumuweka mtu wa karibu ya bwana M.R
kama kawaida yake M Rni mtu anaependa kusafiri ndiyo miongoni mwa sababu za
kujisogeza sana kwa rais na sasa rais safari zake zimezorota kidogo,aliposikiya
kuwa makamu wa kwanza wa rais ataondoka kwenda nchi za ulaya, akaanza mbinu zake
na kuomba kujiunga naye katika msafara huwo akidayi kwenda kumtafuta mgombozi
anayefaa kumgombowa bwa Barutwanayo Amrani meneja mkuu wa redio na televisheni
ya taifa (R T N B)ichukuliwe na Issa Ramadhani anaeshi Gand(belgique)pia ni
katika familiya yake M R na aliwahi kufanya kazi kwenye idara hiyo kabla ya
kwenda huko belgium na kuwa alipita katika shule fulani ya uandishi wa habari
huko kinshasa(RDC)kabla yakuajiriwa (RTNB)haitoshi anafaamika vyema kwa hiyo
itabidi amuone na kumtowa shaka ili akubali kuwa Mkurugenzi mkuu wa RTNB,na kwa
habari za kuaminika katoka kwa watu wa karibu ya Bwana MR nikuwa rais hawezi
kumteuwa kiongozi yeyote yule mpaka aombe ushauri kwa bwanaMR na ndiyo maana
amekuwa ana ahidi mengi na yasiyo wezekana kwa marafiki zake wafedhuli kama yeye,
sasa msichoki bado tutaendeleya kuwapa habari na vituko pia visa vya jamaa.
 |