|
Kambi ya Rukara au kundi la matapeli ?
Le 18 janv. 08
Serikali
imeamua kuambukiza matatizo yake ndani ya jamii,hususani madhehebuni.Na dhehebu
serikali imevalia njuga siku hizi ni lile la Isilam.Katika
kukamilisha dhamira zake ,imeamua kutumia kundi dogo la waislamu ;ambao wana
sifa mbaya katika jamii.Watu hawa wana nia ya kujipatia madaraka kimabavu,pasipo
idhini ya waumini.Maharamiya hawa wamekuwa wakiungwa
mkono na kusaidiwa na Rais Nkurunziza.Hiyi inaonesha dhahiri kwamba
Mheshimiwa Rais, hajatosheka na matatizo aliyopandikiza katika chama tawala ,
vile vile ndani ya chama UPRONA ,ambapo aligonga mwamba.Watu hawa wanatambulika
kwamba ni walafi na wamafia.
Mmoja wao ni Burikukiye Hamza Venant, ambaye ni mwenyekiti wa shirikisho
hewa liitwalo C.I.PE.B, akiwa na lengo la kusaidia yatima.Mradi huo uliungwa
mkono na wafadhili wengi.Lakini kutokana na tabia yake mbaya ya kujigamba na
kutumia pesa za mradi huo isivyo.Mradi huu haukuweza kufika mbali,na hivyo
kujikuta akianguka katika dimbi kubwa la madeni ambayo hakufanikiwa kulipa.
Baada ya huyu mwanachama mwingine ni ; Nibaruta Mohamed El-amin, afisa
mdogo wazamani wa polisi.Huyu amepata umarufu mkubwa kutokana na utapeli
wake.Vile vile ,alianzisha shirikisho ambalo limekuwa ngao ya uharamia wake.Hata
misaada aliyo kupata,ilikuwa ikifikia katika akaunti yake badala ya akaunti ya
shirikisho.Bila haya wala hofu alichukuwa tiketi mbili za ndege za shirika AIR
BURUNDI.kwa niaba ya COMIBU , bila idhini yoyote ya mwenyekiti.Aligushi saini ya
Sheikh Abubakhari Ally, mwenyekiti wa zamani wa baraza la masheikh,kwa
nia ya kuchukuwa fedha kwenye akaunti isiyo kuwa yake.Bwana El-Amini
alitapeli baadhi ya watu ,akidai kwamba atawapatia viza za kwenda ulaya na
Amerika.Hao ni baadhi ya wanachama wa kundi hilo,ambao hawakubaliki katika jamii
ya wa islamu.
Kinara wa kundi hilo ni laana tullah Rukara Mohamed .Alitumia ‘remote
control’ Rais Nkurunziza kuongoza kundi hilo kwa lengo la kusambaratisha jamii
ya waislam.Watu wote hao, hawana wadhifa wowote ndani ya jammi.
Tugependa kufahamisha warundi wote, kwamba waislamu hawana matatizo na madhehebu
mengine hapa nchini.Isipokwa tu chokochoko za kundi hilo na kinara
wao,ambazo zinahatarisha amani ya waislam.
Kumalizia ,tunakumbusha kwamba serikali ya Burundi haina dini ;kulingana na
katiba ya nchi ambayo ilichaguliwa tarehe 28-02-2005,na kutangazwa na Raisi
tarehe 18-03-2005. Kifungo hicho cha katiba, kinakiukwa na Rais pale ambapo
anaanda mihadhara ya injili na kualika viongozi wote wa serikarili ,akitumia
nyenzo za serikali, bila kusahau pesa nyingi anazo chota kwenye akaunti ‘appui
aux bonnes initiatives’Pesa hizo ni msaada kutoka Nigeria, lakini Mheshimiwa
Rais anazitumia kana kwamba zake binafsi.
Burundi Transparence
 |