| Burundi Transparence | |
![]() | |
|
|
|
Site Menu:
| HARAKA HARAKA ZA MZEE MENDE NDIZO ZILITUMA KUPINDUKA MIGUU JUU Le 28 août ‘07 Kama tulivyokuwa tukiwafahamisha ,ikumbukwe kuwa mnamo tareh saba7 Februar 2007 Ndio siku lilofanyika Kongamano la Chama CNDD FDD kinyume na sheria katka Mkowa wa Ngozi. Mtambo wenu wa habari uliweza kuwachambulia haya yafuatayo:
Mkasa uliompelekea Rais wa Jamhuri ambae ni Baba wa taifa kujizunguushia kamba shingoni,umeikosesha nchi muelekeo thabiti na wananchi wake, hata na Chama tawala. Ikapelekea kuzorota shughuli za utawala katika nyanja mbalimbali za Serikali. Kwa uchache hayo yametokana na ushawishi mbaya wa watu waliokuwa wakifika kwenye kasri la Rais,wakiwa na lengo lakusambaratisha Chama kilicho toka msituni na kujipatia madaraka. Walifaanikiwa lengo lao kutokana na viongozi wa ngazi za juu za usalama,kuwa na uchu wakujipatia utajiri wa haraka,bila yakujali maslahi ya wanachama waliokiweka madarakani,nao ni : NSHIMIRIMANA Adolphe,NDAYISHIMIYE Evariste,BUNYONI Allain Guillaume. Wote hao ni maJenerali waliokuwa wapiganaji wa cndd fdd. Wanashindwa kuwajibika kwa kuboresha shughuli za Jeshi na Police ya Taifa,kama ilivyo sainiwa katika Mkataba wa Arusha,wanajishughulisha na kufwatilia wanachama waliokisusa chama cha Rais wa jamhuri kinacho ongozwa na Balozi NGENDAKUMANA Jérémie. Japo chama kilishinda uchaguzi miongoni mwa waliokuwa wakitawala Nchi hii tokea enzi za uhuru,waliona kuwa ushindi huu unakuja kuwakatiza unono waliokuwa wakiupata, hivyo wakaanza kumkashifu ambae waliona kuwa ndie Nuru Kigogo wa chama cha CNDD FDD. Kukawa tetesi za kutoelewana kati ya Rais wa Jamhuri na kiongozi wa chama kipindi hicho. Alakini Muheshimiwa Hon Hussein Radjabu,aliendelea kuwaasa wanachama wa cnddfdd wasijisambaratishe.Wengine waliendeleza uchochezi wao kupitia baadhi ya vyombo vya habari,na mashirika Fulani,matusi yasiokuwa nakifani yakilenga mtuu mmoja tu, kwa lengo la kumshusha hadhi yake.Kukashifu nyadhifa za Serikali nazile za Chama ambazo zilikuwa hazijajidhatiti,ili kuonesha warundi na mataifa kuwa Serikali zote ni sawa. Kutokana na pupa ya kujipatia utajiri wa haraka aliokuwa nao Rais wa Jamhuri nakutokubaini kuwa Adui yake sio yule ambae walishirikiana Vita vya ukombozi, ilimpelekea kutumia uwezo wake kusapoti mpango ambao hakuuandaa yeye, wakusambaratisha Chama tawala cha CNDD FDD chama kilicho muweka madarakani. SIASA Fulani eti:< Ukiukwaji wa sheria unadhohofisha nyadhifa za serikali> Hivi katika utawala kumetanda hofu nakutoelewana,Nyanja zote tatu ambazo ni Bunge,Baraza la Senet na Serikali,hata kitengo cha sheria huwa vinaingiliana bila ya kujuwa kikomo cha majukumu yao,ambavyo nikinyume na Democrasia. Waliochaguliwa wamepoteza muelekeo wakisisasa,inaotokana na mwenendo wa Rais wakuchonganisha nyadhifa ambapo yeye ndie Baba wa Taifa asingelifanya hivyo. Sasa Raia wanasumbuliwa. Ikumbukwe kwamba uongozi wa kanda ulijaribu kushauri uuongozi wa Burundi kwa kila hali bila ya mafaanikio yoyote.Pia twaelewa kuwa Jirani ndie mpatanishi.sasa Burundi imeamuwa kuwa kichwa cha Mwendawazimu?! USALAMA Hofu imetanda katika mio ya warundi na wakaazi wa Burundi,kutokana na mauaji yanayo zagaa kila kona ya nchii mchana kutwa. Vitisho vinavyojitokeza kwa wa Bunge na kunyanyaswa, na wengine kutupwa Gerezani bila ya hatiya kama Hussein Radjabu,sasa Mbunge huo yapata miezi minne katika gereza kuu la Mpimba bila ya hatiya. Shutma za uongo dhidi ya Raia zinazo andaliwa na viongozi wa kuu wa usalama na wale wa chama cha cndd fdd Ngozi cha Rais wa Jamhuri kinacho ongozwa na Jérémie NGENDAKUMANA UCHUMI Kupora uchumi wa Taifa na Rushwa vimetanda Nchini katika nyadhifa za Serikali na zile za Chama tawala. Ikumbukwe mauzo ya Ndege FALCON 50,Utowaji wa Tenda ya Maharage ya ma Polisi. Petrol( Essance) ambayo hutolewa kama Msaada na Nchi ya NIGERIA hakuna anaejuwa kinacho endelea. Kesi ya INTERPETROL imekuwa ni kitendawili. Pia zipo Kesi nyingi ambazo Mbunge Hussein Radjabu hakuweza kuzivumilia, hapo RUJUGIRO na CALIXTE Boss wa InterBank walipo elewana na aliekuwa makamo wa pili wa Rais Bi Alice NZOMUKUNDA wakamkubalia Milliard tatu,ili wauze mali za Serikali ambazo ni OCIBU na BCB wakasaidiwa na BASABOSE Mathias. Hawakuweza kufaanikiwa kutokana na wa Bunge na uongozi wa Chama kipindihicho walisimama imara. Kutokana na Tamaa yakupapua papua,nakukubali kutowa wasivyokuwanavyo,kama nyongeza ya Mishahara hewa, ilikujikweza kwa Raia. Ilipelekea Bank ya Dunia na wahisani pia na FMI kuwaepuka na kuwakana. Habari kutokajijini nikwamba Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao hapa Burundi, Viongozi wakuu wa ma Dini,na Mashirika mbalimbali ya Haki za Binadam, walikuwa wanajuwakuwa Muheshimiwa Mbunge EL Hadj Hussein Radjabu ndie kizingiti cha Maendeleo ya Nchi. Waliendelea kunena kuwa Hussein Radjabu ndie Mwana siasa muadilifu nchini hapa, na wala hakuna Mfano wa wanasiasa walioko hivi hapa nchini kama yeye. Wali muomba RAIS wa Jamhuri amuache huru bila ya sharti lolote lile, sababu hana hatia. Hata baadhi ya waandishi wahabari sasa hawaridhishwi na mwenendo wa Rais wa Nchi hii.
Burundi Transparence
|
|
Burundi Transparence © 2007 | |