Burundi Transparence
main image
shadow shadow

 Actualités


Le 04 octobre 08



Hon. EL-HADJ Hussein RADJABU
Hon. KAMPAYANO Pascaline

Barua N°5
E-mail: iketeryanje@yahoo.fr

Ndugu wananchi wa Burundi,

Na wewe unaowajali na kuwapenda warundi popote ulipo,

Ninayo furaha kupata nafasi hii ili niwaandikie barua hii kuwakumbusha kwamba shujaa alietetea uhuru wa warundi, Mwanamfalme RWAGASORE Louis, aliuwawa tarehe 13 October 1961, na pia shujaa wa demokarasia Raisi Melchior NDADAYE aliuwawa tarehe 21 October 1993. Katika historia ya siasa ya Burundi tunakumbuka kuuwawa kwa vigogo hawa wawili kila mwezi wa Oktoba, ndio maana katika barua hii tutazungumuzia wawo tu, maswala mengine tutayajadili baadae.

Ndugu, RWAGASORE aliuwawa baada ya mwezi mmoja tu wa ushindi wa chama chake UPRONA katika uchaguzi wa tarehe 18 September 1961 na NDADAYE aliuwawa baada ya miezi minne na wiki tatu ya ushindi wake kupitia chama chake cha FRODEBU katika uchaguzi uliofanyika tarehe mosi juni 1993. Chama hicho kilipata pia ushindi katika uchaguzi wa wabunge.

Ndugu,jamaa na marafiki ningependa kuwakumbusha mambo yalionigusa moyoni kuhusu mashujaa hao. RWAGASORE baada ya ushindi wake watu waliotaka kufanya vurugu na kunyanyasa baadhi ya wananchi kwa kupora mali zao kwa kisingizio kwamba wameshinda uchaguzi, RWAGASORE aliwapachika majina ya wazururaji na majambazi, na akatamuka kwamba atakaesubutu kufanya vitendo hivi, utawala wake utamuchukulia hatua kali. Huu ndio ulikuwa ni mwenendo wa serikali yake ili kuwapa haki wapinzani wake. Sasa je, hapo ulipo viongozi waliyo karibu yako ; ukilinganisha na mwenendo wa Rwagasore, wanaofanya vurugu, wanaowatishia wenzao na kuwanyanyasa, kupania kuwatendea maovu kwa visingizio vya kuunga mkono na kukilinda chama tawala, viongozi hawo huwachukulia hatua gani watu hawa? Kama hawafuati mfano wa shujaa huyo, basi ni mambo ya aibu kwa sababu shujaa huyu baada ya ushindi wa chama chake, alisema ushindi huwo sio wa chama tu, bali ni wa wananchi wote. Na kuhusu utawala bora na maendeleo, aliwambia warundi kwamba yeye na wenzake waliopo madarakani watatambulika zaidi kutokana na mema watakayoyatenda. Na endapo warundi wataridhika, basi yeye na wenzake watasherehekea. Mwenzangu, usitake kusifia kiongozi ili umufurahishe tu, ama viongozi wasitake kupewa sifa wakati ambapo mema kutoka kwao hayaonekani.Ebu tizama, watu wanafungwa hovyo, wengine wananyanyaswa, njaa inatesa, na kadharika.

Ndugu,jamaa na marafiki kama mnamfahamu NDADAYE anawakumbusheni nini ? Endapo haujawahi kumusikia acha nikueleze machache kumuhusu yeye. Mimi nilipata nafasi ya kumufahamu. Kumbuka kwamba nilikuwa Mbunge niliechaguliwa kutoka chama cha FRODEBU katika Mkoa wa Ngozi. Ningependa kukumbusha kwamba hata kama chama cha UPRONA hakikuweza kubabaishwa na yeyote yule mwaka 1961 kutokana na ujasiri wa Mwanamfalme RWAGASORE, mwaka 1993 mambo yalikuwa mengine. Katika pirika pirika za kuandaa uchaguzi, aliyekuwa waziri wa mambo ya Ndani, NGEZE François, na mwenye madaraka makubwa ndani ya chama cha UPRONA wakati huwo, alitoa vitisho vikali dhidi ya wakuu wa mikoa na viongozi wa matarafa, na viongozi wa vyombo vya usalama. Idadi kubwa ya warundi walifungwa na kunyanyaswa kwa ajili ya kutofuata sera za chama UPRONA. Licha ya hayo, alitishia kukifuata chama cha FRODEBU baada ya kugundua kwamba kuna ugumu wa kupambana na fikra za NDADAYE. Hapo sasa, NDADAYE alifahamisha kwamba chama chake ni kama maporomoko ya maji hakuna yeyote anayeweza kuyazuia. Na katika sherehe za kuapishwa baada ya ushindi, NDADAYE alitamka haya, nilikuwepo ndani ya ukumbi wa mikutano ya wabunge wa Kigobe, kwamba yeyote atakayejaribu kuzuia demokarasia atakuta mamilioni ya wananchi wamesimama imara(bwuma kwa rugha ya Taifa, yaani kama chuma) wakitetea hayi zao. Baada ya kuuwawa kwake wapo ambao walilitafsiri neno hili kinyume kwa malengo ya kuchafua jina lake. Siku zijazo, nitapata nafasi ya kuwaelezeeni maana yake, pamoja na maneno kama vile « gususuruka », yaani kupata joto. Nitawafahamisha tena maana ya neno lingine tunalolitumia « umuka », yaani nyauka, na mengine mengi.

Ndugu, RWAGASORE na NDADAYE ni mashujaa wa demokarasia walioturithisha kupiga vita uongo, uonevu, dharau na usaliti, kwa hilo basi nachukua nafasi hii ili nimshukuru Mheshimiwa Mbunge El-Hadj Hussein RADJABU aliyetunga wimbo mnawoufahamu na kuingiza ndani maneno hayo ambao baadhi ya wenzetu wanauimba kwa aibu (wimbo wa chama cha CNDD-FDD). Kwa kumalizia, nawaomba mnisaidie kulaaani na kupiga vita uuzwaji na ubinafsishaji kinyume cha sheria wa mashirika ya serikali. Hayo tutayajadiri siku za usoni, leo nimeyagusia tu kwa sababu hata uwanja wa kaburi ya shujaa NDADAYE inasemekana kwamba umeuzwa. Mwenyezi Mungu awasaidie viongozi hao na warundi sote pia kufuatilia na kuenzi mfano bora wa mashujaa hawo.

Ahsante.

                                          Hon. KAMPAYANO PASCALINE
                                                  

Burundi Transparence

 

 

 

horizontal bar

 

Burundi Transparence © 2008