Actualités
Le 17 septembre 08

Hon. EL-HADJ Hussein RADJABU
Hon. KAMPAYANO Pascaline
Barua N°2
E-mail: iketeryanje@yahoo.fr
Ndugu wananchi wa Burundi,
Na wewe unaowajali na kuwapenda warundi popote ulipo,
Kwa mara nyingine tena, pokea salamu zilizojaa kheri. Hofu niliyokuwanoyo kuhusu mchakato mzima wa amani ya Burundi umenifanya niwasiliane na wewe.
Unafahamu kwamba kuna mkataba wa kusitisha mapigano kati ya serikali ya Burundi na chama cha palipehutu-FNL uliosainiwa tarehe 6 Septemba 2006.
Kwa hiyo, pakiwemo na jeshi la serikali, kundi la FNL ambalo ni la tisa lililokuwa likitarajiwa kuingiza wapiganaji wake ndani ya vyombo vya ulinzi
na usalama, huku wanasiasa wao wakijiunga na vyombo vingine vya utawala nchini kulingana na mkataba huo. Majadiliano ambayo tulitegemea yanakaribia
kumalizika na tulifikiri kwamba tu mbioni kupumua, sasa limefufuka kundi lingine la kumi ambalo serikali imekiri kulitambua na kutegemea kurishirikisha
kama makundi mengine katika mpango huu wa amani pamoja na kuwa halitambuliki kimataifa. Kumbuka ya kwamba wabunge waliweka wazi dosari kuhusu uundaji
wa kundi hilo. Hata hivyo, serikali kujisogezea watu wake siyo vibaya, ikiwa itapata uwezo, sababu hadi sasa Benki ya Dunia inaonekana kutojishughulisha
na kundi hilo. Nanyi ndugu kutoka nchi mbali mbali mnaoetupenda na bado mnajaliwa na Mwenyezi Mungu afya njema, na pia mliyechangia kutusuruhisha na
kutupa moyo. Ninyi ni mashahidi ya yaliojadiliwa popote pale palipofanyikia mazungumuzo. Tupe ushauri sisi na serikali yetu sababu tupo njia panda.
Tuweke wazi makosa ya serikali ili yapatiwe ufumbuzi,hii haimaanishi kuipinga bali ni kuipenda.
Ndugu mwananchi, ikiwa ulishauri ama ulichukua hatua ili vijana toka kundi hilo waandaliwe kuingizwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, nipe nieleze
faida ulioiona ya kundi hilo ili niweze kuelewa kwamba ni faida ya kitaifa. Kutoelewa kwangu kunasababishwa na kutokuwepo kwa mkataba unaoweka wazi
uhusiano wa kundi hilo na serikali. Naulizia tena; waliostaafishwa katika jeshi la ulinzi na polisi ilikuwa ni mbinu za kutafutia nafasi vijana kutoka
kundi hilo? La sivyo, je wako watakaopunguzwa ili vijana hawo wapate nafasi? Ni upi umuhimu wakuingizwa kundi hilo katika vyombo vya usalama kuliko wale
watokaoingizwa kutokaa na mkataba?
Waheshimiwa Raisi wa nchi na Mwenyekiti wa chama cha Palipehutu-FNL, tuokoeni mtekeleze mkataba pasina kwenda kinyume nao ili tupate afueni angalao kuhusu
usalama. Mrundi ndugu, hofu nilio nayo ni h iyo tu. Kama ulikuwa na hofu kama mimi, tuvumliye kwa imani na tutarajie kwamba ushauri wa wanaoipenda Burundi
utatusaidia.
Umuhimu wa habari hii haukunipa nafasi ya kukueleza hali ya Mbunge El-Hadj Hussein Radjabu kama nilivyo kuahidi ila, fahamu tu kwa siku ya leo kwamba afya
yake ni njema na anaendeleza vizuri fungo zake za mwezi mtukufu wa Ramadhani. Namalizia kwa kukufahamisha kwamba habari zilizotangazwa kuwa hakuweza kupokea
tume ya uchunguzi kutoka bungeni kwa uuzaji wa ndege Falcon 50 zina dosari. Fahamu kwamba hakupata mwaliko wowote ule kutoka bungeni. Nitakapo pata nafasi
nyingine nitakufahamisha ni nini kilitokea ili asiweze kuzungumuza na tume hiyo.
Ahsante, Mungu awe nanyi!
Hon. KAMPAYANO PASCALINE
Burundi Transparence
 |