Burundi Transparence, c'est l'actualité en continue.
Accueil                     Précedente                     Suivante                 Archives

 

 

 Actualités

Mgombea urais Burundi atiwa mbaroni Dar
(Source: Nipashe)  
 Le 14 janvier 12

Aliyekuwa mgombea wa urais wa Chama cha MSD cha nchini Burundi, Alexis Sinduhije, jana alifikishwa katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akiwa amefungwa pingu pamoja na ulinzi mkali wa askari polisi wenye bunduki.

Sinduhije aliyekuwa amevaa suruali ya jeans ya rangi ya bluu na fulana nyekundu, alifikishwa mahakamani saa 3:14 asubuhi akikabiliwa na tuhuma za mauaji.

Habari za kuaminika, ambazo NIPASHE ilizipata mahakamani hapo, zilidai kuwa Sinduhije, ambaye pia ni Mwenyekiti wa MSD, alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere (JNIA) wakati akiingia nchini na kufikishwa kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama hiyo, Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda, Sinduhije hakusomewa mashtaka kutokana na maelezo yaliyotolewa dhidi yake kuwa na upungufu ambapo alirejeshwa kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Hata hivyo, saa 6:11 aliondolewa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi na haikufahamika mara moja kama alipelekwa kituo gani cha polisi.